GET /api/v0.1/hansard/entries/780623/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780623,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780623/?format=api",
"text_counter": 47,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mohamend Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13455,
"legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
"slug": "mohamed-ali-mohamed"
},
"content": "Kaunti ya Kilifi ina madaktrari wa upasuaji wa caesarean section 18. Ina madaktari wa upasuaji 18 peke yake. Idadi ya vitanda ni 610. Wagonjwa wanaokwenda kutibiwa kila siku ni zaidi ya 10,852. Watu wanaokufa ni 1,410. Wanakufa kwa sababu ya magonjwa ya kiajabuajabu. Magonjwa yanayo tiba lakini tunayachukulia mzaha mzaha. Leo, Mombasa tunakufa kwa sababu ya Chikungunya; eti ukiumwa na mbu, wewe kwisha. Hatuna wataalamu wa kupambana na magonjwa. Maradhi ya ajabuajabu yanatokea na hatuwezi saidika. Asilimia kubwa ya Wakenya hata hawana ile Bima ya Afya ya Kitaifa. Hawawezi kujitetea na hawajui la kufanya. Angalia Kaunti ya Mombasa. Idadi ya wanaokufa ni 1,272. Katika miaka ya 2014 na 2015, Kilifi ilifanyia upasuaji wagonjwa 2,668. Waliokufa ni 1,553. Haikubaliwi. Inasemekana kwamba kila nafsi itaonja mauti, lakini suala la kuonja mauti kwa sababu ya udhalimu na uzembe wetu sisi Wabunge halikubaliki. Sisi ni wasomi ambao tuko na Bachelor’s Degree na"
}