GET /api/v0.1/hansard/entries/780627/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780627,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780627/?format=api",
    "text_counter": 51,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mohamend Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13455,
        "legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
        "slug": "mohamed-ali-mohamed"
    },
    "content": "ambayo ni hatua ya kwanza ya daktari kuingia. Mshahara wao wa kwanza wakimaliza mafunzo ni Kshs44,000. Daktari aliyekaa katika taaluma hiyo kwa muda wa kati ya miaka 10 na 15 – daktari ambaye anakuangalia tu hivi na anajua dawa yako – analipwa Kshs114,000 katika Kenya ya sasa. Ndio unaona tumekuwa na uhaba wa madaktari. Wengi wao wanakimbia kwenda kufanya kazi nje. Wengi wanafungua hospitali zao za kibinafsi ambazo haziwezi kufikiwa. Daktari aliye na uzoefu wa zaidi ya miaka 15 analipwa takriban Ksh200,000. Watu wanaumia na wanakufa. Sisi tuna uwezo. Mungu hatusamehi sisi Wabunge kwa sababu tukiwa wagonjwa tuna suluhu. Sisi tunaenda katika mahospitali ya kifahari. Tunapanda ndege na kuenda Ulaya kutafuta matibabu lakini Mungu anaturegesha katika majeneza na masunduku hadi nchini Kenya. Kisha tunaanza kupiga kelele na kusema kwamba ni vipi Mbunge fulani alipelekwa nje aende apate matibabu amerudi akiwa maiti? Ni aibu. Hatuwezi kutunga sheria za kuleta hospitali, usawa na haki? Leo sisi tunasikia uchungu mmoja wetu akituondokea kwa sababu tumejaribu kila tuwezacho. Tumetumia pesa, tumemwaza Nairobi Hospital, Aga Khan Hospital, tumempandisha ndege, ameenda Uingereza na Marekani lakini hivyo hivyo, amerudi akiwa maiti ndani ya sanduku. Yule mama anayeuza mboga kule Kaloleni, Giriama; yule mama anayeuza viazi kule Nyeri; yule mzee ambaye anakaa kule mashinani Turkana na Pokot; ni nani anayempeleka katika hizi hospitali? Ni nani anayemkatia nauli ya kupanda ndege na kuenda Ulaya? Hakuna? Atakayefanya hiyo kuhakikisha ya kwamba watu hawa hawatapata haya matatizo ni sisi Wabunge wote. Kwa kauli moja, tukubaliane ya kwamba hii ina umuhimu zaidi na ni ya Wakenya asilimia 80 ambao hawana huduma za afya. Leo nchini Kenya, miaka 55 baada ya kupata Uhuru, mama anajifungua ndani ya nyumba. Jamani hatuoni haya? Jamani hatuogopi Mungu? Mama anakufa akijifungua mimba kwa sababu hawezi kufikia hospitali. Mfano ni katika Eneo Bunge la Nyali, ninakotoka. Linaonekana kama eneo Bunge tajiri kwa sababu ukisema unaenda Nyali watu wanajua ni Eneo Bunge tajiri. Lakini utashangaa nikikuambia kwamba Mungu anajalia akina mama wetu kupata mimba ndani ya Nyali lakini wanajifungua katika Eneo Bunge la Mvita. Hali hii haikubaliki."
}