GET /api/v0.1/hansard/entries/780639/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780639,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780639/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kanini Kega",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1813,
"legal_name": "James Mathenge Kanini Kega",
"slug": "james-mathenge-kanini-kega"
},
"content": "Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niafiki Hoja hii ambayo imeletwa na rafiki yangu, Mheshimiwa wa Nyali, Mohamed Ali, ambaye tunamjua sana kwa jina “Jicho Pevu”. Tunafurahia kwa sababu Hoja ambayo amewasilisha hapa ni muhimu sana, na yale aliyoyaangazia ni mambo ambayo yanaathiri watu wetu kila uchao. Lakini wakati Mhe. Ali jana alipokuwa anatoa Hoja hii, angetoa ilani kwa Wabunge kwamba leo tutakuwa tunaongea kwa Kiswahili ndiyo watu waweze kubeba kamusi. Nimeona sana wakati Mheshimiwa alikuwa anaendeleza Hoja hii, wengi walikuwa wameachwa vinywa wazi. Hawakuwa wanaelewa, hasa sisi ambao tumetoka bara. Lakini nitajaribu nione kama nitaweza kuiafiki Hoja hii kulingana na matarajio ya Mhe. Mohamed Ali. Tutakumbuka kwamba wakati tulipoanzisha serikali za ugatuzi mwaka wa 2013, tuliona sana magavana wengi wa nchi hii wakikimbia kununua magari ya kusafirisha wagonjwa yanayojulikana kwa kimombo kama ambulance . Walikuwa wanazinunua ili wakipata wagonjwa katika sehemu zao, waweze kusafirishwa mpaka kwenye hospitali kuu hapa Nairobi na kule Eldoret. Kuhusu uzima wa mwili, yani health, kwa maoni yangu, tulikosea kidogo wakati tulipoigatua sekta hiyo. Labda sekta hiyo ingeshikiliwa na Serikali ya kitaifa, haswa tukizingatia kwamba kila kuchao sisi, kama Wabunge, tunaitwa kushirika kwenye mikutano ya kuchangisha pesa. Hizo fedha tunachanga kila siku ni za kupeleka wagonjwa hospitali, ama ni za kugharamia kuzikwa kwa maiti? Vifo vingi vinavyotokea katika taifa hili husababishwa na magonjwa ambayo yanaweza kutibiwa ama kuhudumiwa kabla ya kusababisha vifo. Haya magojwa yatatibiwa namna gani ilihali hatuna hata zahanati? Yatatibiwaaje kama hatuna madaktari na waauguzi? Yatatibiwaaje kama madaktari tulionao nchini... Tuna madaktari ambao wanahitimu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}