GET /api/v0.1/hansard/entries/780641/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780641,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780641/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kanini Kega",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1813,
"legal_name": "James Mathenge Kanini Kega",
"slug": "james-mathenge-kanini-kega"
},
"content": "Mhe.Naibu Spika wa Muda, naomba sisi kamaWabunge lazima tufanye kazi yetu sawasawa na tuhakikishe kwamba waliotuchagua, walituchagua tuwashughulikie kiafya, ajira na mengine. Mhe. Mohamed Ali alisema hospitali za rufaa ni muhimu sana. Tuko na mbili, moja hapa Nairobi na ingine kule Eldoret. Tukiangazia maeneo ya uwakilishi Bunge, hasa nikitoa eneo langu la Bunge kama mfano, hatuna hospitali ya kiwango cha 4, hata hospitali ya kiwango cha 5. Tuko na zahanati peke yake. Wagonjwa kutoka eneo langu la uwakilishi Bunge wanasafirishwa zaidi ya kilomita 200 ili wapate huduma za afya. Lazima tuimarishe zahanati tulizonazo kule mashinani ili zile za kiwango cha 4 ama kiwango cha 5 zihudumie wagonjwa ambao hawapati huduma kule mashinani."
}