GET /api/v0.1/hansard/entries/780656/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780656,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780656/?format=api",
    "text_counter": 80,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wakhungu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1889,
        "legal_name": "Chrisantus Wamalwa Wakhungu",
        "slug": "chrisantus-wamalwa-wakhungu"
    },
    "content": "Vile vile, tuko na Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta ambayo inajali masilahi ya wagonjwa kutoka eneo la Kati, Nairobi na eneo la Mashariki. Vile vile, hii Hoja ya kuwa na Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa kule Mombasa itasaidia sana kwa sababu kuna wagonjwa wengi wanaotoka kaunti za Lamu, Mombasa, Kwale, Kilifi na Taita Taveta. Ukiangalia ajenda ya jubilee, utapata kwamba matibabu yamepewa kipaumbele. Isitoshe, kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo, hasa lengo la tatu (SDG-3), mambo ya universal healthcare yamezingatiwa. Mwenzangu Mohamed Ali ameongea kiswahili mufti. Tulijaribu kumfuatilia ikawa vigumu lakini katika zile pilkapilka za kumuelewa tukagundua kwamba tunaendelea kujifunza kidogo kidogo."
}