GET /api/v0.1/hansard/entries/780660/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780660,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780660/?format=api",
    "text_counter": 84,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wakhungu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1889,
        "legal_name": "Chrisantus Wamalwa Wakhungu",
        "slug": "chrisantus-wamalwa-wakhungu"
    },
    "content": "Hii Hoja ikipita, yafaa aifuatilie ili tuwe na Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa kule Mombasa.Wengine labda wanasema Mombasa si Kenya. Sisi tunajua Pwani ni Kenya. Ni vizuri hospitali iwe hapo karibu ili iwasaidie akina mama, watoto na wagonjwa kwa ujumla. Wakenya wanatumia pesa nyingi kuenda ng’ambo kutafuta matibabu. Wengine wanaenda kule India ilhali matibabu wanayotafuta huku yanapatikana hapa nyumbani. Ukienda kule Kenyatta, wagonjwa wamejaa sana. Tukitaka hospitali ya Kenyatta isiwe na wagonjwa wengi, lazima tuanzishe hospitali nyingine za rufaa. Kule Eldoret, kuna Hospitali ya Rufaa na Mafunzo. Tunataka hospitali ya rufaa kule Mombasa ijengwe ili wagonjwa wa saratani waende pale. Vile vile, upasuaji utafanywa pale."
}