GET /api/v0.1/hansard/entries/780666/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780666,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780666/?format=api",
    "text_counter": 90,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wetangula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 3036,
        "legal_name": "Timothy Wanyonyi Wetangula",
        "slug": "timothy-wanyonyi-wetangula"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nami pia nichangie Hoja hii ya Mhe. Mohamed Ali ambaye kwa umaarufu anaitwa “Jicho Pevu.” Hii ni Hoja ya maana sana. Katika nchi hii yetu, miaka 54 tangu tujinyakulie uhuru, suala la afya bado linatuchanganya. Tunatumia pesa nyingi sana kupeleka wagonjwa katika nchi za nje kutafuta matibabu. Hizi pesa zinaweza kutumika katika nchi hii kujenga hospitali ambazo zinaweza kuwa na vifaa maalum.Tuko na madaktari ambao wamehitimu katika nchi yetu wanaoweza kufanya kazi katika hizi hospitali. Ukienda Hospitali Kuu ya Kenyatta, utapata kwamba haina vifaa vya kisasa. Hii ni aibu kubwa. Madaktari wapo lakini wale wanafanya upasuaji wanafanya kazi katika mazingira duni kabisa. Lazima tuweke maanani mambo ya afya kwa sababu nchi ambayo haina afya haiwezi kuendelea. Nchi ambazo zimeendelea zimetilia mkazo sana mambo ya afya. Kitu kingine ni kwamba matibabu katika nchi yetu ni ghali sana. Watu wanalipa pesa nyingi. Ndiyo maana unapata watu wanakufa kwa magonjwa ambayo yanaweza kutibiwa. Wagonjwa wengi hawawezi kufika hospitali ama wakifika hospitali huwa hakuna madawa. Lazima Serikali iekeze pesa katika mambo ya afya ili tulipe madakdari vizuri, tununue vifaa, tuweke madawa katika hospitali na tujenge hospitali za kisasa katika kila kaunti, vile Mhe. Mohamed amesema. Tuko na kaunti 47. Kaunti nyingi hazina hospitali za kiwango cha 4 yaani Level 4. Nyingi ni hospitali ndogo ambazo hazina vifaa vya kisasa. Karibu miaka 20 iliyopita nilipopata ajali, nilipelekwa Brussels, Ubelgiji kwa matibabu. Nikienda huko, nilifikiria ninaenda kupata matibabu ambayo hayawezi kupatikana hapa Kenya. Nilipofika huko, niliona mambo ya kawaida ambayo yanafanywa hapa Kenya. Kwa sababu hatuna hospitali ya kiwango cha juu, singepata hayo matibabu huku kwetu. Mimi ninajua kuna wakenya wengi ambao wanapata ajali katika barabara zetu na hawawezi kufika hospitalini kwa sababu ni ghali na hakuna vifaa vya kusaidia wagonjwa ambao wamepata matatizo ya uti wa mgongo ama wale wa saratani. Ukienda hospitali za kibinafsi kama Aga Khan ama Nairobi utapata wako na vifaa vya kisasa ambavyo vinaweza kutibu aina yote ya magonjwa lakini ni wakenya wangapi wanaweza kufika katika hizo hospitali? Kwa hivyo, hii Hoja itawezesha kujengwa hospitali ambazo zitafikiwa na wananchi wa kawaida. Vile vile, Serikali inatakikana iangalie gharama ya matibabu kwa sababu matibabu katika zile hospitali za umma inashinda watu. Watu wakienda huko, daktari anawaandikia dawa ama vifaa vya kununua ili warudi kutibiwa. Hiyo haiwezekani kwa sababu wananchi wengi wana The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}