GET /api/v0.1/hansard/entries/780667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780667,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780667/?format=api",
    "text_counter": 91,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wetangula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 3036,
        "legal_name": "Timothy Wanyonyi Wetangula",
        "slug": "timothy-wanyonyi-wetangula"
    },
    "content": "matatizo mengi. Kuna umaskini na tunatakikana tuangalie kwamba watu wanapata matibabu badala ya kuambiwa waende watafute matibabu pahali pengine. Tukijadili hii Hoja, tunatakikana tuifanye sheria katika nchi yetu ili tuanze kufikiria ni namna ipi tutainua viwango vya mahospitali ili tuwe na hopitali ya Level 5 katika kila kaunti; iwe na vifaa vya kisasa, dawa na ile huduma ya madaktari kutumwa huko. Kila wakati tuna migomo ya madaktari. Madaktari wa Hospitali ya Kenyatta wamefanya upasuaji hivi juzi na kutibu mtoto ambaye mkono wake ulikuwa umekatika lakini hakuna mtu anawatambua . Wakifanya kosa kidogo, utaona kila mtu anawaelekezea kidole cha lawama. Madaktari wanang’ang’ana kufanya kazi katika mazingira duni. Lazima tuangalie ni vipi tutafanya bidii tuweke kiwango cha hospitali zetu kiwe katika hali nzuri."
}