GET /api/v0.1/hansard/entries/780672/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780672,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780672/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Tuya",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 926,
"legal_name": "Roselinda Soipan Tuya",
"slug": "roselinda-soipan-tuya"
},
"content": "Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja hii nzuri sana. Ningependa kuanza kwa kumpongeza Mtoahoja, Mhe. Mohamed Ali Mohamed. Nilipokuwa nikimsikiza akiwasilisha Hoja hii, niliona kwamba alipoingia kwenye siasa, lile jicho lake pevu bado liko pale pale. Nasema hivi kwa sababu amewasilisha Hoja ambayo ameifanyia utafiti wa kutosha na kutupa njia muafaka ambayo kila mmoja ambaye anajali afya ya waliotuchagua kuwa Wabunge wa Bunge la Kitaifa, bila shaka sote tutaunga mkono Hoja hii. Nilipokuwa namsikiza Mhe. Ali na ukiangalia Hoja yake, haiangazii tu hali ya Kaunti ya Mombasa. Mtoahoja ametuelekeza kwa Kifungu cha 25 ambacho kinatukumbusha ya kwamba kuna lile azimio ambalo tumetoa tukiwa watungasheria au wanasheria la kuwa na maono ya kuhakikisha katika kila gatuzi la nchi hii kuna ile Hospitali ya Kitaifa ya Kiwango cha 6. Nikiunga mkono Hoja hii, nimekuwa mmoja wa wale wa Bunge la 11 ambao walihuzunishwa na kule kuweka maslahi ya afya yawe kwenye serikali za kigatuzi na kuyaondoa kwa Serikali kuu. Sababu yangu ya kuona hapo hatukufanya vyema ni ukijaribu kuangalia mpangilio wa kazi wa kaunti zetu jambo la afya liko chini kabisa kwa orodha ya umuhimu katika kaunti zetu. Nilisikia mmoja wa Wabunge ambao waliongea mbele yangu akisema kwamba mipangilio ya magavana wengi wamekimbilia kununua yale magari ya dharura ama ambulances . Tayari hiyo inaonyesha yale mawazo yaliyo kwa magavana wetu. Wazo lao ni kwamba kile wanakipa kipaumbele ni njia ya kuwaondoa sehemu gatuzi zao na kuwapeleka nje ya zile kaunti ili kupata matibabu. Hiyo inatuonyesha kwamba yale mamilioni ya pesa wameweka kwa kununua yale magari yangewekwa katika kuweka msingi ama kuweka hospitali zinazopatikana katika kaunti ziinuke kuingia kwa hali nyingine. Katika Kaunti yangu ya Narok ambapo mimi ndiye mwakilishi wake, ukienda kwa ile hospitali kuu ambayo tuko nayo katika Kaunti ya Narok, hali yake ni ya kutatanisha zaidi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}