GET /api/v0.1/hansard/entries/780673/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780673,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780673/?format=api",
"text_counter": 97,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Tuya",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 926,
"legal_name": "Roselinda Soipan Tuya",
"slug": "roselinda-soipan-tuya"
},
"content": "Utakuta kuna daktari lakini mgonjwa akitaka kufanyiwa utafiti zaidi analazimika kutoka pale kwa hospitali kupelekwa na jamaa yake kutafuta pahali pa kutoa damu ili ipimwe kwingineko. Kununua dawa, inalazimika atoke kwa hospitali akatafute dawa kwingine. Nafikiri hiyo ni kuonyesha kwamba mipango yetu ama kwa lugha ya Kimombo priority zetu hatuzajiweka vizuri kama nchi. Kifungu cha 43 cha Katiba yetu kinaruhusu ama kuweka wazi ya kwamba kila Mkenya anastahili kuwa na kiwango cha juu zaidi cha afya bora. Ni haki, si ndoto au kitu tunatarajia kupata. Kwa sasa, iko katika ile sehemu tunaita Bill of Rights ambayo kila Mkenya anahitajika kuwa nayo. Ukiangalia ule utafiti ambao Mhe. Mohamed ameufanya na kutuonyesha vifo ambavyo vinafanyika katika hospitali zetu za kaunti unaonyesha kwamba hali yetu ya afya inazidi kuzorota siku baada ya nyingine. Hata kama tungekuwa tunataka kufanya mabadiliko ya kidharura, bado nafikiria twahitaji kulifikiria jambo la afya; tuone kama tunaweza kulirudisha kwa Serikali ya juu ili liangaziwe na kupewa uzito unaostahili. Tukiendelea hivi, Wakenya watazidi kufa kiholela na kwa magonjwa madogo madogo ambayo yanaweza kutibiwa. Tutazidi kuona kwamba afya itakuwa inapatikana na wale ambao wanajiweza kiuchumi tu."
}