GET /api/v0.1/hansard/entries/780674/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780674,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780674/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Tuya",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 926,
"legal_name": "Roselinda Soipan Tuya",
"slug": "roselinda-soipan-tuya"
},
"content": "Hiyo si halali, ni kinyume na Katiba yetu. Hivi juzi, shida ilitokea katika hospitali kuu ya Kenyatta. Watu wakapata shida kule Garissa, Wajir na sehemu nyingi nchini, tumekuwa na shida nyingi za kiafya kama vile shida za akina mama kudhulumiwa kwa njia mbalimbali. Tumaini waliyo nayo ni kutolewa kule waliko wapelekwe katika hospitali kuu ya Kenyatta. Wakati hospitali hiyo inapopata shida, kama kupata “homa” au “kupiga chafya”, Wakenya wote hupata “homa” na kila mmoja anaitegemea hospitali hiyo; pamoja na Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Eldoret. Hatuwezi kuendelea hivi. Umefika wakati ambapo tunafaa kujadiliana na kuliangazia suala la afya kwa lengo la kubadili mipangilio yetu katika sekta hii. Kwa hivyo, nampongeza Mhe. Mohamed, ambaye ndiye mwasilishi wa Hoja hili. Naunga mkono kubuniwa kwa hospitali ya kiwango cha sita kule Mombasa. Ninaomba juhudi hizo pia zifuatilishwe katika kila sehemu gatuzi humu nchini kwa sababu hiyo ndio sheria tunayotunga. Hivi sasa, sioni kama mtu yeyote anayefikiria vizuri anaweza kuipinga Hoja hii. Sisi sote tunaunga mkono. Hoja hii itashughulikiwa na Kamati ya Utekelezaji, si Kamati ya Implementation kama alivyosema, Mhe. Spika. Hii itahakikisha kuwa Hoja hii imeenda katika kiwango kingine ili kuhakikisha Hoja hii…"
}