GET /api/v0.1/hansard/entries/780676/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780676,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780676/?format=api",
"text_counter": 100,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ng’ongo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 110,
"legal_name": "John Mbadi Ng'ong'o",
"slug": "john-mbadi"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchangia Hoja hii. Kwanza kabisa, ningependa kumkosoa mwenzangu, Mhe. Wamalwa, ambaye amesema sina uwezo wa kuzungumza Lugha ya Kiswahili. Pengine sina uwezo wa kuzungumza Lugha ya Kiswahili sanifu lakini nina uwezo kama Mkenya mwingine yeyote kuzungumza Lugha ya Kiswahili, kwa sababu hii ni lugha ya taifa. Pia ningependa kuwajuliza kwamba mimi nilisomea Lugha ya Kiswahili hadi kidato cha nne. Nilipitia katika somo la Kiswahili. Nilipokuwa nikiwania kiti cha Bunge, wawaniaji wenzangu walifanyishwa mtihani wa Lugha ya Kiswahili; lakini mimi nilipewa ruhusa kwa sababu nilifanya mtihani wa Lugha ya Kiswahili katika kidato cha nne. Kwa hivyo, si kweli kwamba Mhe. Mbadi hawezi kuzungumza Lugha ya Kiswahili. Sasa ningependa kuchangia Hoja iliyoko mbele yetu. Kwanza, ningependa kushukuru mwenzangu, Mbunge wa Nyali kwa kuileta Hoja hii Bungeni. Katika Kifungu cha 43 cha Katiba yetu, afya imepewa uzito zaidi. Kifungu hiki kinasema kwamba kila Mkenya ni lazima apate The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}