GET /api/v0.1/hansard/entries/780677/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780677,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780677/?format=api",
"text_counter": 101,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ng’ongo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 110,
"legal_name": "John Mbadi Ng'ong'o",
"slug": "john-mbadi"
},
"content": "matibabu ya kiwango cha juu zaidi ambayo yanaweza kupatikana humu nchini. Kwa sababu hiyo, inatakikana tuangalie sana sekta hii, kama nchi. Nimesikia wenzangu wakisema kwamba pengine sisi kama Wakenya tulifanya makosa kupeleka sekta ya Afya kwa serikali za ugatuzi. Natofautiana nao kwa sababu ugatuzi ulikuja hivi juzi tu; mwaka wa 2013. Kabla ya ugatuzi, huduma za afya zilikuwa chini ya Serikali ya kitaifa kwa zaidi ya miaka 50, na kupata huduma za matibabu ilikua shida sana. Hii ndiyo sababu sisi Wakenya tuliamua huduma hii ni lazima iwekwe kwenye serikali za ugatuzi ili sisi wenyenye kule mashinani tuone jinsi tutakavyoshughulikiwa. Haistahili tuwe na hospitali ya kiwango cha sita Mombasa pekee. Kama Wakenya, inatakikana tuliangazie suala hili kwa nia nzuri na tutafute fedha ili tujenge hospitali za kiwango hicho katika maeneo yote humu nchini; yakiwemo Kisumu, Kakamega na hata Garissa, ili watu wetu wakipata magonjwa yasiyoweza kutibiwa katika hospitali za kawaida, waweze kutibiwa haraka na karibu. Ningependa kuwahimiza Waheshimiwa wenzangu kuunga mkono Hoja hii, na pia tuifuatilie. Tusiipitishe tu halafu ikuwame hapo tu. Kamati ya Bunge husika iko na jina gumu sana. Nilimsikia mwenzangu akijaribu kuibatiza kamati hiyo jina la “implementshoni”. Ni Kamati ya Utekelezaji. Tunamuomba mwenyekiti wa kamati hiyo, tutakapoipitisha Hoja hii leo ama baadaye, wahakikishe kwamba maombi ya mwenzangu yametekelezwa. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninaunga mkono."
}