GET /api/v0.1/hansard/entries/780687/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780687,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780687/?format=api",
    "text_counter": 111,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, ni wazi kwamba jinsi mienendo na mitindo ya kimaisha inavyobadilika, kumekuwa na changamoto nyingi sana hasa za kiafya. Kwangu binafsi, tungekuwa na uwezo wa kurudisha masaa nyuma tungelipitisha Hoja hii juzi. Waswahili husema kuwa “Hayawi hayawi huwa.” Kwa hivyo, ninaonelea kuwa ni Hoja ambayo wakati wake ni huu. Mambo kuhusu afya katika nchi yetu ya Kenya yanatatanisha sana. Kama vile walionena mbele yangu walivyonena: Walalahoi, afya yao imeachwa mikononi ya Maulana. Pia, Mwenyezi Mungu aliweka tofauti kati ya binadamu na ng’ombe kwa kutupa akili kama ya kutibu ili tuitumie kisawasawa. Ni jambo la aibu kwamba Wakenya wengi wanakatika maisha mapema. Maisha ya wale ambao wanalinda familia zao yamekatika kwa ghafla. Wale wanaowategemea huachwa wasiwe na mbele wala nyuma. Hii ni kwa sababu gharama ya matibabu iko juu sana. Watu wanalazimika kuuza mifugo wao na hata mashamba ili kugharamia matibabu. Isitoshe, wagonjwa wanapoaga dunia, wanaobaki huwa hawana mbele wala nyuma. Wabunge katika Bunge hili watakubaliana nami kuwa kila Ijumaa tunaitwa katika michango hapa na pale kwa ajili ya kuchangia wagonjwa. Kwa hivyo, Hoja hii aliyowasilisha Mheshimiwa “Jicho Pevu” ni Hoja ambayo imewasilishwa wakati bora na itatulazimu tuache shughuli nyingine zote ili tuipitishe; kisha tuhakikishe imetekelezwa."
}