GET /api/v0.1/hansard/entries/780688/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780688,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780688/?format=api",
    "text_counter": 112,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, jimbo la Mombasa anakotoka mwanzilishi wa Hoja hii, ni jimbo ambalo linasifika kwa utalii. Watu wengi ambao wanastaafu haswa wale ambao wanastaafu katika nchi nyingine na wanaathiriwa na baridi ya nchi zao, huja kupumzika kule Mombasa. Hawa ni watu ambao wako na taaluma tofauti tofauti wakiwemo madaktari. Tutakapokuwa na hospitali ya rufaa kule Mombasa, itasaidia pia watalii wagonjwa. Leo hii mtu akitoka Laikipia akitaka kutibiwa anaingia gari la moshi la Standard Gauge Railway (SGR) ambayo ililetwa na Serikali ya Jubilee, moja kwa moja mpaka Mombasa kutibiwa. Kwenda Mombasa si kama kwenda India kutafuta matibabu."
}