GET /api/v0.1/hansard/entries/780689/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780689,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780689/?format=api",
"text_counter": 113,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": "Cha kutia aibu sana ni kwamba katika Karne ya 21, akina mama wanakufa kwa ajili ya kujifungua. Katika hospitali zetu za majimbo bado hatujajimudu kuhakikisha kwamba akina mama wanapoleta maisha duniani humu, hawapotezi maisha yao. Kwa hivyo, tunapozungumzia mambo ya afya, ni sharti pia tuelewa kwamba taifa lenye afya ni taifa tajiri. Iwapo wale watu ambao sisi tunaongoza watakuwa wana afya njema, basi tutaweza kuwaambia vijana wetu wajitafutie riziki. Wataweza kufanya hivyo bila kuhangaishwa na maradhi."
}