GET /api/v0.1/hansard/entries/780690/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780690,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780690/?format=api",
    "text_counter": 114,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "Ni jambo la kutia hofu sana kwamba kila mara tunalia nchi haina fedha ilhali fedha nyingi zinapotelea katika miradi isiyofaa na yenye kufaidi watu binafsi. Hiyo ni miradi ya kuendeleza ufisadi. Ninazungumza bila kusita kwa sababu najua tulitenga fedha katika Bunge hili ili zitumike katika ugatuzi kwa kununua vifaa vya hali ya juu vya hospitali. Vifaa hivyo vilinuiwa kusaidia wagonjwa ambao wanalazimika kusafiri hadi Nairobi kupata matibabu. Kwa mfano, kusafishwa damu. Magonjwa kama vile kisukari, mpigo wa damu na saratani yamekithiri. Kwa hivyo, tuansema hivi: Iwapo kuna fedha zitatengewa masuala ya matibabu, basi fedha hizo zitumike vilivyo na kikamilifu kama alivyosema mwenye Hoja. Aliongeza kusema kwamba tumekuwa tukitia gunia pumzi. Baadhi ya majimbo, tunapozungumza sasa hivi, yamehifadhi mashine zilizogharimu mabilioni ya pesa katika mahospitali. Pesa zilizotumika si kwamba zimetoka kwenye mfuko wa mtu binafsi, bali ni kodi ambayo wamelipa Wakenya."
}