GET /api/v0.1/hansard/entries/780694/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780694,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780694/?format=api",
    "text_counter": 118,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Maanzo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2197,
        "legal_name": "Daniel Kitonga Maanzo",
        "slug": "daniel-kitonga-maanzo"
    },
    "content": "Asante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa muda wa kuchangia Hoja hii muhimu sana inayohusu mambo ya afya. Mheshimiwa Mohammed Ali Mohammed amafanya jambo la busara sana kuangazia mambo ambayo yanawahusu Wakenya wengi. Kulingana na Katiba yetu katika Kifungu cha 43 na mpangilio wa kwanza wa sheria ya afya ya mwaka wa 2017, inaashiriwa kuwa kutakuwa na hospitali za kitaifa za rufaa za kiwango cha sita katika kila ugatuzi. Ni muhimu tulijadili suala hili na tuhakikishe limetekelezwa, kwa sababu kila sehemu ya ugatuzi nchini inafaa kuwa na hospitali kama ile ya kitaifa ya Kenyatta, ambayo sasa hivi inawashughulikia wagonjwa kutoka pande zote za nchi. Kuna hospitali nyingine kama hiyo kule Eldoret. Ni hizo mbili tu tunazo katika nchi yetu. Zitahitajika zingine 45 kote nchini. Ningependa kuwapongeza magavana ambao wameshughulikia mambo ya afya na wamejaribu sana kutengeneza hospitali ambazo wako nazo. Mfano ni sehemu ya ugatuzi ya Makueni. Tumeshikana na Gavana wetu, Kivutha Kibwana ili kushughulikia mambo ya afya. Nimeona vile vile kuna magavana wengine ambao wanajaribu sana kuhakikisha kuwa afya imeendelezwa katika sehemu zao za ugatuzi. Hata hivyo, ni lazima Serikali kuu ihakikishe kwamba hospitali nyingine kama Kenyatta zimebuniwa na zimetengenezwa katika gatuzi tofauti tofauti. Sasa hivi hospitali ya Kenyatta inapokea watu kutoka kila mahali nchini. Imekuwa vigumu kuwasaidia wagonjwa wote katika hospitali hiyo. Hata ulinzi unakuwa ni shida kupeanwa. Kuna mgonjwa mmoja kutoka Eneo Bunge langu la Makueni ambaye aliibiwa pale hospitalini katika sehemu ya kupokea huduma za dharura. Hii inamanisha kwamba hata ulinzi umekuwa changamoto. Kwa hivyo, ni vyema Hoja kama hi iangaziwe. Aidha ni muhimu pesa itengwe kwa ajili ya masuala ya afya. Ikibidi, tutafute fedha kutoka kwa wafadhili ambao wanaweza kutusaidia. Hivyo, tutaweza kujenga hospitali katika magatuzi yetu likiwemo gatuzi la Mombasa. Kuna maeneo ya ugatuzi tofauti huko Pwani. Kuna Taita Taveta Kaunti na gavana wa huko anafanya juhudi kubwa ndiyo hata huko kuwe na hospitali kubwa, lakini fedha za kutosha hazijapatikana. Pia, kuna Kwale Kaunti na Mombasa Kaunti kwa Gavana Hassan Joho ambaye pia anaweka bidii lakini bado fedha hazitoshi. Vile vile, kuna Kilifi Kaunti na eneo hilo lote linatakikana liwe na hospitali moja kubwa haraka iwezekanavyo."
}