GET /api/v0.1/hansard/entries/780702/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780702,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780702/?format=api",
    "text_counter": 126,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Leo hii, mapendekezo hayo yatatusaidia. Kwa mfano, kule kwangu Jomvu kulitokea matatizo makubwa sana katika sehemu ya Owino Uhuru ambako kulikuwa na athari ya sumu. Tuliona huko Mombasa Kaunti kupitia Gavana Ali Hassan Joho walijaribu kuwatibu wananchi ambao waliathirika na hiyo sumu. Mpaka sasa, kwa shauri hakujakuwa na hospitali kubwa ya kuweza kuwatibu hao watu, bado athari hizo zimeongezeka. Leo hii, ukiangalia watoto ambao wanazaliwa, wengine wamedua. Pia wazee wanatamani kupata watoto wengine lakini mayai yao hayafanyi kazi vizuri. Kwa hivyo, watoto hawawezi kupatikana."
}