GET /api/v0.1/hansard/entries/780703/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780703,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780703/?format=api",
"text_counter": 127,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Kwa hivyo, Hoja hii ni nzuri sana. Tukiwa na hospitali ya rufaa tutaweza kutekeleza mambo mema kama yale ya ndugu yangu Mhe. Wamalwa ya utekelezaji. Utakuwa ni utekelezaji wa ukweli kupitia kwa kamati. Katiba yetu katika Kifungu cha 43 kinasema kwamba kila Mkenya ana haki ya kupata matibabu. Kwa hivyo, tukiwa na hospitali ya rufaa huko Mombasa haitatosha. Ni muhimu, hospitali hizi ziwe Kenya nzima ili tuone Wakenya wakiishi katika hali nzuri ya kuweza kupata matibabu kama haki yao ya kisheria. Tumeona ndugu yangu Mohamed Ali amechanganua vizuri kabisa na kusema madaktari Kenya nzima ambao wamesajiriwa ni 11,000. Lakini, wale wanaofanya kazi ni karibu 6,000 pekee. Kwa hivyo, tukiangalia hali hii haiwezi kutupeleka mbele. Madaktari wako lakini The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}