GET /api/v0.1/hansard/entries/780704/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780704,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780704/?format=api",
"text_counter": 128,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "hawawezi kukimu yale mahitaji ya mamilioni ya watu ambao wako Kenya. Kwa hivyo, tukiangalia hali hii ya kuwa na madaktari wachache humu nchini, tunaona tunawapeleka wagonjwa hospitalini na baada ya siku chache tunawaona hao wagonjwa wakirudi katika hali ambayo si sawasawa. Ndugu Mohamed Ali amesema kwamba, ni kweli Wabunge matumbo yakiwatokota kama vile mtambo wa kusaga unga, wanapata njia ya kuweza kukimbia ulaya na sehemu nyingine kwa sababu wana huduma za bima na mambo mengine. Vile vile, hata tumbo la Spika nalo likitokota kama vile mashine ya tuk tuk, vile vile anaweza kwenda ulaya kupata matibabu. Lakini mwananchi wa kawaida hawawezi kukimu matibabu hapa nchini. Kwa hivyo, pendekezo langu ni kwamba pesa ziende mpaka huko mashinani. Wale wote ambao hawawezi kulipia huduma ya kitaifa ya bima tuone kuwa watu hawa katika nyanjani wanaweza kulipiwa ili watu wote katika Kenya nzima wawe na bima. Tukiangalia katika ajenda kubwa nne za Serikali ya Jubilee ya Raisi Uhuru Kenyatta, hilo ni jambo moja ambalo wamelitia maanani sana. Kwa hivyo, pendekezo langu ni kwamba, kwa sababu madaktari wetu ni wachache, wale wanaofanya katika mikataba waweze kuajiriwa kazi."
}