GET /api/v0.1/hansard/entries/780708/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780708,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780708/?format=api",
    "text_counter": 132,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Wiki mbili zilizopita, nilizungumzia kuhusu shida ya maji na leo naungana na ndugu yangu Mhe. Maanzo, kusema kwamba magonjwa mengi sana yanaletwa na shida ya ukosefu wa maji. Kama vile ilivyo katika Kipengele cha 43 cha Katiba yetu, kila mmoja ana haki ya kupata huduma ya afya. Vile vile, kila mmoja ana haki ya kupata maji safi katika nchi yetu ya Kenya. Jomvu kwangu watu wanaumia kwa sababu ya ukosefu wa maji safi. Ni muhimu sana tushikane na washikadau wote katika nchi hii kuona kuwa tumewapatia maji safi wananchi wetu ili hali yao ya afya iwe nzuri. Tusipofanya hivyo, katika kuwaelimisha watu wetu kuwa katika hali nzuri, kila watakapokuwa wagonjwa tukiwapeleka hospitali itakuwa ni kama vile ule msemo wa Kiswahili unaosema kuwa itakuwa “kirba goji, goji kirba;” yaani, twaenda humo humo na twajirudisha humo humo. Kwa hivyo, ni vizuri kuona kuwa tunawalea watu wetu katika hali nzuri ili waweze kujisaidia katika hali ya sawasawa. Pia, nataka kusema kuwa mambo ya matibabu hayapendi siasa wala chukuchuku. Kwa hivyo, ni muhimu sana sisi wanasiasa tuwaunge mkono wataalamu ambao wanafanya kazi zao katika hospitali. Ni vizuri kuwatetea na kuangalia kile ambacho hawana katika hospitali ili tuwasaidie wawe nacho ndio waweze kutoa huduma bora kwa wananchi wetu wa Kenya. Kuna kelele nyingi siku hizi. Katika Kenyatta National Hospital kumetokea matatizo kama Mbunge mwenzangu, Mhe. Wanyonyi, alivyozungumzia. Leo matatizo yametokea na watu wanaruka wakitaka Waziri Sicily Kariuki aende nyumbani. Nataka kusema kitu kimoja kwa huyu waziri. Ana siku mbili au tatu alizokuwa katika afisi ile. Kwa hivyo, jambo la muhimu ni kuacha kuingilia mambo ambayo hatujakuwa na utaalamu zaidi. Tunamuunga mkono Waziri Sicily The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}