GET /api/v0.1/hansard/entries/780709/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780709,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780709/?format=api",
"text_counter": 133,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Kariuki na tunataka afanye kazi yake bila kumuingilia. Na penye matatizo tusi- mvictimise bali tuhakikishe kwamba amefanya kazi yake vizuri na hospitali hizo zimepata dawa na kuweza kuendelea kuwahudumia Wakenya. Kwa hivyo, namuunga mkono ndugu yangu, Mhe. Mohamed Ali, Mbunge wa Nyali; kwa kuleta Hoja hii na kuona kuwa Hoja hii haitarudishwa nyuma. Kamati ya Utelekelezaji ifanye juhudi kuona kuwa yale tuliyoyafanya yametekelezwa. Serikali, kupitia Kamati ya Bajeti, ione kuwa pesa zimetengewa shughuli hii. Kando na kuwa na Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Eldoret na hii ya hapa Nairobi, sisi watu wa Mombasa tungependa kujivunia kuwa na hospitali ya rufaa. Ninasema hivyo kwa maana gavana wangu, Mhe. Ali Hassan Joho amejizatiti katika Hospitali ya Coast General, Mombasa. Ameirekebisha na kuitengeneza lakini mpaka dakika hii, tukiangalia hospitali ile, haiwahudumii watu wa Mombasa peke yake. Inawahudumia watu kutoka sehemu tofauti tofauti. Kwa hivyo, Serikali inapaswa kutuma pesa ili tufungue hospitali ya rufaa na tusaidiane na magavana wetu ili wananchi wetu wapate huduma bora ya afya. Kwa hayo machache, namuunga mkono Mhe. Mohamed Ali, na kusema Wabunge wengine tuchangie na kuunga mkono Hoja hii ya matibabu."
}