GET /api/v0.1/hansard/entries/780713/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780713,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780713/?format=api",
    "text_counter": 137,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Tum",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 913,
        "legal_name": "Tum Tecla Chebet",
        "slug": "tum-tecla-chebet"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, nataka kuunga mkono Hoja hii iliyoletwa na Mhe. Ali. Tunajua kwamba Kipengele cha 25 cha Katiba ya Kenya na Kipengele cha kwanza cha Sheria ya Afya vinasema kwamba tutaweka hospitali ya rufaa katika kila jimbo. Nataka kusema kwamba watu wanakufa wengi sana kwa sababu hawana dawa na vifaa ambavyo vinafaa katika hospitali zetu. Hoja hii itawasaidia Wakenya sana. Sisi Wabunge tunaitwa kila wiki kushughulikia watu wengi ambao wako na shida. Tuko na magonjwa mengi kama ugonjwa wa saratani, ugonjwa wa figo na watu wameuza mashamba wakabaki hohehahe. Hawawezi kuwapeleka watoto wao shuleni kwa sababu wanalazimika kwenda kupata huduma kwenye hospitali za kibinafsi na kulipa Kshs4 milioni. Inabidi mtu auze shamba lake la ekari tano ili apatiwe dawa zinazofaa. Tunajua kwamba tuko na hospitali mbili za rufaa. Tuko na moja kule Eldoret na pia tuko na ile ya Kitaifa ya Kenyatta. Tunajua kwamba hospitali ya Mombasa inahudumia kaunti sita. Tumeona kuwa watu wa Mombasa wanataabika sana na tunaiunga mkono Hoja hii. Tunajua kwamba kama kuna shida katika hospitali wanaoteseka ni kina mama. Kwa nini ninasema kina mama wanateseka? Kina mama wako na kazi nyingi kule nyumbani. Baba wa nyumba akiwa mgonjwa, mama wa nyumba huacha kila kitu kuhakikisha kwamba watoto wameenda shuleni. Tunajua kwamba katika hospitali zetu za kaunti hakuna dawa wala mitambo ya kuwashughulikia watu wanaougua ugonjwa wa figo. Hatuna mashine za kuwashughulikia watu wenye ugonjwa wa saratani. Tunaweka hii iwe priority number one katika nchi yetu ya Kenya. Tunajua Serikali ya Jubilee iko na ajenda nne. Moja ya hizo ni kupatia kila mmoja matibabu ya kufaa. Tukitaka kuendeleza hii ajenda tuanzishe hospitali za rufaa katika kaunti The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}