GET /api/v0.1/hansard/entries/780714/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780714,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780714/?format=api",
"text_counter": 138,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Tum",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 913,
"legal_name": "Tum Tecla Chebet",
"slug": "tum-tecla-chebet"
},
"content": "zote. Tangu tulipopata Uhuru mwaka wa 1963, tuliapa kwamba tutaangamiza matatizo ya ugonjwa, upumbavu na umaskini. Lakini umaskini unachangiwa na kutokuwa na hospitali za rufaa. Hali hiyo inasababisha watu kuuza ardhi yao ili waweze kupata huduma katika hospitali za kibinafsi. Hakuna Mbunge ambaye halii. Mimi kama mama kaunti wa Nandi ninaitiwa harambee ishirini kila mwishoni mwa wiki. Tunaomba Serikali itusaidie kwa sababu kupeana dawa na kila kitu ni kazi ya Serikali. Mshahara mdogo tunaolipwa hautoshi kisimamia harambee ya kuchangia watu. Hii ni kwa sababu ya magonjwa, kuchangia watoto wa shule na kila kitu. Utaona Mbunge akijiongelesha peke yake kwa sababu hawezi kupata pesa za kumchangia mtu aliyelazwa hospitali. Ninaomba tuweke maanani afya ya watu wetu. Tupitishe yale Mhe. Ali amesema. Na haitakuwa Mombasa peke yake, kwa sababu watu wetu wanakufa sana. Tuwe na hospitali za rufaa katika kila kaunti na tuweze kutimiza ajenda moja ya Serikali ya Jubilee. Asante."
}