GET /api/v0.1/hansard/entries/780720/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780720,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780720/?format=api",
    "text_counter": 144,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadime",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "Kabla hata sijaongea, kwa kweli na dhati kabisa, naunga mkono hii Hoja. Kabla sijasahau, najua wenzangu hapa wameongea kuhusa masuala ya maji. Nadhani katika awamu ya Bunge la 11, nilipitisha Hoja ya maji na Wabunge hapa waliunga mkono kwa wingi kabisa kuwa kila taasisi ya umma ipate maji. Hiyo Hoja ilipita vizuri lakini kwa sasa hivi mpaka dakika hii hatujui imefiki wapi. Nimejaribu kuifuatilia kila mahali lakini ninatupwa huku na kule. Kwa hivyo, Kamati Tekelezi ni vyema ifuatilie hiyo Hoja. Ikiwezekana maji ipatikane kila mahali ndiyo magonjwa mengi yapungue."
}