GET /api/v0.1/hansard/entries/780721/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780721,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780721/?format=api",
    "text_counter": 145,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadime",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "Kwa sasa hivi, mimi kama mwakilishaji wa Eneo Bunge la Mwatate naona saratani inatumaliza. Na ni kweli watu wengi sana wana saratani. Juzi tu, nilikuwa na Mbunge wa kwanza ambaye alikuwa anawakilisha Eneo Bunge la Mwatate. Alikuwa anateta na kuuliza kwa nini Bunge isifanye bidii ili kila kaunti angalau ipate mashine ya kuangalia saratani. Mwenzangu wa Nyali, Mhe. Ali, kwa kweli hii Hoja ameitunga na ikatungika. Tunasema tutaifuatilia ili itekelezwe. Kama vile Mbunge wa Jomvu alivyosema, tusikuwe na mambo ya mchezo maanake magonjwa kwa kweli hayataki siasa. Wakenya tutakuwa tumesaidika. Mwanzo tuanze na ile mikoa ya zamani nane. Kila mkoa angalau upate hospitali ya rufaa, na vile vile tuangazie kila kaunti."
}