GET /api/v0.1/hansard/entries/780728/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780728,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780728/?format=api",
    "text_counter": 152,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Dawood",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2572,
        "legal_name": "Abdul Rahim Dawood",
        "slug": "abdul-rahim-dawood"
    },
    "content": "Tuna changamoto kwani hatuna madaktari. Hata wakati nilikuwa nikileta Hoja yangu, tulikuwa tunasema hatuna madaktari. Mhe. Mohamed Ali ametuambia leo kwamba madaktari wanalipwa pesa kidogo. Lazima tufikirie ni kitu gani tutawafanyia madaktari wetu. Hatutakuwa na madaktari kila siku, wanaenda kwa hospitali kisha wakirejea nyumbani hawana pesa kwa mfuko. Wanafanya kazi kutoka asubuhi mpaka usiku na hata ukiwapigia saa nane ya usiku unatarajia wakuwe hospitalini, lakini hawana fedha. Tukiwa nchi na Wabunge, lazima tufikirie Kenya yetu inaenda vipi. Tunaelekea vizuri ama la? Kama hatuna afya kama Kenya nzima, basi hatutaendelea mbele."
}