GET /api/v0.1/hansard/entries/780729/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780729,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780729/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Dawood",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2572,
"legal_name": "Abdul Rahim Dawood",
"slug": "abdul-rahim-dawood"
},
"content": "Nashukuru, Mhe. Ali amesema tunaweza kujenga hospitali na Kshd3bilion, na tuziboresha zile zilizoko ili ziwe hospitali za rufaa na Kshs2bilioni. Nauliza ni nani anatoa hizo pesa, kama sio Bunge kutenga hizo pesa ziende kwa hospitali? Katika Kaunti yangu ya Meru, tulikuwa na hospitali ya Level 5. Kwa wakati huu, Gavana wetu, Hon. Kiraitu, anaipeleka ikuwe Level 6. Nasikitika miaka 15 iliyopita, tulikuwa na mashine ambazo zilitoka Spain lakini hatuna wataalamu wa kuzitumia. Katika Kenya yetu, lazima tutafute wataalamu ili mashine zilizoko kwa hospitali ziweze kutumika. Nashukuru Serikali ya India kwa kutupatia mashine ya babatron mwaka uliopita ya kuangalia saratani. Lakini tujiulize kweli kama mashine moja ndiyo itafaa Kenya nzima ambayo ina idadi ya watu 45milioni. Serikali na Bunge, lazima tupitishe pesa zile na ziangaliwe zisikuwe na sakata ya ufisadi, kama zile za Afya House ambapo tunasikia Kshs5 bilioni zinapotea. Wale wamechukua hizo pesa lazima wachukuliwe hatua na tusiwadhulumu madaktari. Wiki mbili ama tatu zilizopita, daktari katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta alifanya upasuaji mtu asiyefaa. Kama angekimya, nani angejua amefanya vibaya? Hakuna mtu angejua. Ni vizuri alisema amekosea. Sasa tusiwalaumu hao. Waziri Cecily Kariuki amesema hajafuta kazi yule Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta, Ms. Lily Koros. Amesema akae kando ndio mambo yaangaliwe kwa sababu Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta ina shida nyingi. Lazima tuone tutakavyofanya. Lakini tukisema kwamba tutampeleka nyumbani kwa sababu ya kumfuta ‘mtu wetu’… Kwani nani siyo mtu wetu? Kila mtu Kenya hii ni mtu wetu! The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}