GET /api/v0.1/hansard/entries/780734/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780734,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780734/?format=api",
    "text_counter": 158,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. King’ara",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": "Asante sana Naibu Spika wa Muda, kwa jicho lako la ujasiri kwa kuniona na kunipatia mwanya wa kuchangia mjadala huu ulio na uzito mkali, kama vile ulitangulia kusema pale mwanzo. Kila mtu hapa ameguzwa kwa njia moja ama nyingine na masuala ya kiafya. Si mzaha kusikia joto kali kutokana na usemi wa kiongozi wetu kutoka Mombasa, “Jicho Pevu”. Na ni jicho pevu halisi. Ni vizuri kutilia uzito mkuu masuala ya afya kuliko mambo mengine yoyote yale. Ni afya njema imetuwezesha kuja hapa na hata kutupatia nguvu ya kucheka. Langu ni kuwakumbusha Wabunge na Wakenya kwa jumla kuwa Kenya iko na maeneo matatu makubwa: Nairobi, Mombasa na Kisumu. Eneo la Mombasa ni njia moja ya kuingia katika nchi yetu. Kuna njia tatu za usafiri: anga, ardhi na maji. Mombasa ndiyo eneo kubwa sana la kuingiza mizigo katika nchi yetu. Tumepata gari moshi la kasi hivi juzi. Ingekuwa bora ikiwa tungepata mambo mengine kwa mwendo wa haraka, kwa mfano mambo ya kudumisha afya njema. Kama vile mwenzangu amenena hapo mbeleni, Mombasa inaathiri maeneo mengi. Ni vizuri tuwe na hospitali kubwa ya rufaa katika eneo la kisiwa cha Mombasa. Kuna wengine walichangia hapa kuwa katika vyuo vikuu hapa nchini, tunafunza madaktari wengi sana lakini wakimaliza masomo yao, hawafanyi kazi hapa kwetu. Ni vizuri sisi Wabunge tujiulize kwa nini watu wetu wanasoma na hawatuhudumii. Wengi wameenda kufanya kazi ughaibuni. Je, huko ughaibuni kuna nini ambacho hatuna hapa? Kwa nini sisi tukaachwa nyuma? Sisi Wabunge inastahili kutenga hela za kuziimarisha hospitali zetu. Na kama vile wengine wamesema, kama tumepata ugatuzi, kwa nini tusipate ugatuzi rasmi kwa mambo yote, hasa kiafya? Nimetoka Ruiru, si Mombasa. Eneo langu liko na watu 600,000. Katika hospitali kuu hapo Ruiru, akina mama hujifungua watoto 26 kila siku. Hata leo watapatikana. Vitanda vya watoto ni 12. Vitanda vya wanaume ni saba peke yake. Je, hayo ni maendeleo kweli? Sharti turudi nyuma kidogo tuchunguze ni wapi tulipotea na kuacha kuzingatia masuala ya afya katika nchi yetu. Hakuna mtetezi wa wanyonge! Asante sana ndugu yangu, Mhe. Mohamed Ali Mohamed, kwa kujitokeza kuwatetea wanyonge. Wale watu maskini waliotupatia kura tukajipata hapa Bungeni ndio wasioweza kujitetea. Wacha tuchukue fursa hii tuwatetee ndio wapate mwanya wa kuishi maisha mazuri kama sisi. Hiyo itapatikana tukiunga mkono mjadala huu kwa kishindo ili mambo mazuri yapatikane kwa hawa wanyonge. Nilikuwa na hofu kidogo wakati tumekaa hapa Bungeni tukiongea kuhusu mijadala muhimu iliyo na maendeleo mwafaka katika nchi yetu. Kulikuwa na upinzani kidogo hapa. Hapa tumepata mwanya mzuri sana wa kufanya kazi kama kikundi kimoja. Kwa vile upande wa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}