GET /api/v0.1/hansard/entries/780735/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780735,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780735/?format=api",
    "text_counter": 159,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. King’ara",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": "Upinzani na sisi katika upande huu mwingine tunaongea kwa lugha moja kuhusu maendeleo, basi mimi naona hata hii hospitali itajengwa haraka hata kuliko anavyotarajia ndugu yangu. Hilo likifanyika, basi litakuwa limeambatana na zile ajenda nne zilizopendekezwa na kiongozi wetu wa Jubilee, Uhuru Kenyatta. Sitasahau kuwakumbusha kwamba hata katika zile hospitali chache za rufaa tulizonazo, vifaa vya matibabu havipo. Ndiyo maana unaona watu wengi bado wanaenda ng’ambo. Hata kama tutachangia na kujenga hospitali za rufaa, itabidi sisi Wabunge tutenge fedha zitakazotumiwa katika utafiti wa magonjwa hasa yale yanayotuathiri. Kenya ni nchi ambayo imeendelea kama mnavyojua. Sijui ni nini twakosa hata tukashindwa kujimudu kimaisha hasa kiafya? Kama mnavyojua, Wakenya wote wanatuangalia sisi Wabunge wao. Kwa hivyo, si King’ara hapa peke yake - Hata wewe, pahali popote pale uwakilishapo, mwananchi anakuangalia na afya yake iko mikononi mwako. Hii ni kwa sababu wewe ndiwe umehitimu kuwatetea na kuleta mijadala kama hii ambayo itawapatia afya njema kule mashinani na mijini. Sitasema mengi kwa vile nataka kuwapa muda wengine ambao wamekuwa wakingojea tangu asubuhi kama mimi. Naunga mkono Hoja hii na kushukuru sana kwa vile upande wa Upinzani umetuunga mkono kufanya kazi pamoja kama Wakenya."
}