GET /api/v0.1/hansard/entries/780754/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780754,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780754/?format=api",
"text_counter": 178,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. ole Sankok",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13166,
"legal_name": "David Ole Sankok",
"slug": "david-ole-sankok"
},
"content": "Tuko na shida pia ya migomo ya madaktari. Hawagomi bure. Madaktari sio kama wafanyikazi wengine wa Serikali. Wanafanya kazi masaa 24. Wanaitwa usiku wa manane, kwa mfano, kushughulikia mgonjwa ambaye labda walimtibu mchana lakini hakupata nafuu na anataka kuonana na daktari aliyemtibu wakati wa mchana. Inabidi daktari huyo amke ili aende kazini. Tunapoteza madaktari kwa sababu nchi jirani wanalipa madaktari vizuri kuliko Kenya. Kwa hivyo, inatakikana pia tufikirie tutambue shida yetu. Tunatoa mafunzo kwa madaktari wengi katika vyuo vikuu. Siku hizi, Chuo Kikuu cha Kenyatta na kile cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta vimeanzisha mafunzo ya udaktari. Pia tuko na wauguzi wanaosomea vyuo vya mafunzo ya uuguzi. Lakini ukitembelea hospitali zetu za Serikali, unapata hao madaktari hawafanyi kazi huko. Wengi wao wamefungua hospitali za kibinafsi kwa sababu ladba wanapata pesa. Wengine wamehamia nchi za kigeni. Inabidi tuhakikishe madaktari wanahudumu kwa hospitali zetu za serikali. Watu wote hawana uwezo wa kuenda kwenye hospitali za kibinafsi kwa sababu ya gharama ya juu. Ni uchungu sana ukiona mama akibeba mtoto afikishe kwa hospitali lakini daktari hawezi kumsaidia kwa sababu hana dawa. Ikiwa kuna vifaa ambavyo havipatikani kwenye hiyo hospitali, daktari anamtuma huyo mama anunue hivyo vifaa ama dawa kwenye maduka ya madawa lakini huyo mama hana uwezo. Daktari anaangaliana na mama mpaka mtoto anakufa mkononi mwa mama kwa sababu ya ukosefu wa vifaa katika hospitali zetu. Ni uchungu mkubwa. Sisi ambao tunatunga sheria tuko na uwezo wa kupelekwa ng'ambo tunapokua wagonjwa. Tumeona watu ambao wamepelekwa ng'ambo kuwekwa bandeji pekee wakigongwa kidogo na mawe. Kuna wenzetu ambao wanakufa kwa ugonjwa ambao unatibika. Katika karne hii, ugonjwa wa malaria unaua watu humu nchini licha ya kwamba tuko na aina zote za dawa za malaria. Unakuta ugonjwa wa pnuemonia unaua watoto nchini Kenya ilhali tuna dawa za kukabiliana na magonjwa kama hayo. Kwa vile madawa hayo hayapatikani kwa urahisi katika hospitali za umma, matibabu yanakuwa ni kwa watu walio na pesa. Kulingana na Kifungu 43 cha Katiba yetu, afya bora ni haki ya kila Mkenya. Siku hizi afya bora ni haki ya walio na pesa, na siyo haki kwa wasio na pesa. Ni lazima tulitilie maanani na tulizingatie suala zima la afya. Ninataka pia kumwambia Mhe. Ali kuwa tukishaipitisha Hoja hii, afuatilie kuona kuwa imetekelezwa. Ikibidi urudi Bungeni ili tuweze kutoa maagizo, afanye hivyo ndiyo masuala yanayoshughulikiwa na Hoja hii yasiishie hapa Bungeni. Hii itatuwezesha kuhakikisha maombi yote tunayoyapitisha hapa Bungeni yametekelezwa iliWakenya wote waweze kupata matibabu. Hata kama nimeongea Kiswahili ambacho kidogo kinatatiza, ninajua kwamba nimejikakamua. Mhe. Omollo, ahsante kwa kuja kutuunga mkono. Umemaliza kazi yako. Sasa nitakuwa nikipambambana na nani? Sasa kazi yangu imeisha. Hiyo handshake imemaliza kazi yangu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}