GET /api/v0.1/hansard/entries/780756/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780756,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780756/?format=api",
    "text_counter": 180,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Baya",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13373,
        "legal_name": "Owen Yaa Baya",
        "slug": "owen-yaa-baya"
    },
    "content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Nimesimama kuunga mkono Hoja ambayo imeletwa na ndugu yangu Ali ambaye anatoka eneo la Pwani. Hospitali ya rufaa ya kiwango cha sita huko Pwani imechelewa kufika. Mimi ningependa kuongea kwasababu hospitali hii ya Mombasa iwekwe kama hospitali ya rufaa. Kwanza, kuna magonjwa mengi hapa duniani ambayo huathiri watu wanaoishi Pwani. Ni magonjwa ambayo hayawezi kufanyiwa utafiti katika maeneo mengine. Matibabu yake yanafanyika vizuri yakifanyiwa pale Pwani. Saa hii pale Mombasa, kuna ugonjwa wa Chikungunya, ambao unaathiri wapwani peke yao. Kuna magonjwa mengine kama vile tende guu ambayo yako katika eneo la Pwani peke yake, na matibabu yake hayawezi kupatikana mahali pengine popote humu nchini. Kwa hivyo, kama tunataka kuwasaidia watu wa Pwani na kuhakikisha kwamba wamepata haki yao ya kikatiba, kulingana na Kipengee 43 cha Katiba, ni haki kwamba hospitali ya Mombasa ifanywe hospitali ya rufaa. Pili, hospitali ya Mombasa imekuwa pale muda mrefu kabla hospitali nyingine hazijajengwa humu mchini. Pengine Hospitali Kuu ya Kenyatta peke yake ndiyo inatoshana na hospitali ya Mombasa ki-umri. Hospitali ile imesahaulika licha ya kwamba ni hospitali ambayo wakati wa ukoloni na baada ya kupata Uhuru ilitiliwa maanani sana. Hospitali hiyo ilikuwa ikopewa kila kitu lakini ikafika wakati ikaachiliwa. Sasa, tuko na wakati mwafaka kwa sababu ya kile ndugu yangu Sankok alichokitaja kuwa handshake. Sasa tunataka ile handshake pia ifike kule Pwani ili tuone matunda yake.Tunataka ile hospitali ya Mombasa iwe tunda la kwanza la ile handshake. Sisi Wapwani tutafurahi. Pengine ningefanya ukarabati wa hii Hoja kusema kwamba haya mambo yawekwe katika Bajeti ya mwaka huu wa kifedha ili tuhakikishe kwamba hospitali ya rufaa ya Mombasa inatimilika. Tatu, hospitali ile inasaidia kaunti karibu nane za Kibwezi, Lamu, Tana River, Taita Taveta, Kilifi na maeneo mengine. Watu wote huteremka Mombasa kutafuta matibabu. Zaidi ya watu milioni kumi nchini huenda kwenye hospitali ile kutafuta matibabu lakini ukiangalia ambulensi ambazo zinaenda Mombasa, zote huelekea kwenye hospitali za kibinafsi, ambazo zina gharama kubwa kwa watu wetu. Jambo lingine ambalo ningependa kusema ni kwamba kuna ugonjwa wa saratani ambao umekithiri zaidi Mombasa na sehemu ya Pwani kwa jumla, kwa sababu ya madini mazito ama heavy metals yanayopatikana katika eneo lile. Utafiti unaonyesha kwamba watu wengi katika Kaunti yaKwale wameathirika kutokana na ugonjwa wa saratani. Katika kaunti ya Kilifi, kwa sababu ya kuweko kwa madini mazito aina ya iron ore na titanium, ambayo yako na carbon, wakazi wanaathirika kutokana na ugonjwa wa saratani kwa urahisi kuliko wakazi katika sehemu zingine za Kenya. Kwa sababu hiyo, na kwa sababu ya uchafuzi wa hewa unaofanyika Mombasa, tunahitaji usaidizi wa haraka ili hospitali ya Mombasa iweze kupandishwa cheo na kuwa hospitali ya rufaa. Nikimalizia, kwa sasa kuna utafiti ambao unafanywa. Pale kwetu kilifi, kuna kitengo kinaitwa Kenya Medical Research Institute (KEMRI) ambacho kinafanya utafiti wa tropical diseases. Ule utafiti kwa sasa umeonyesha kuwa watu wengi wa Pwani wanaathirika na tropical diseases ambazo matibabu yake hayapatikani humu nchini. Tukifanya hospitali ya Mombasa kuwa ya rufaa na kuweka vyombo ambavyo vitatuwezesha kupata matibabu ya magonjwa hayo, itakuwa tumefanya jambo la busara. Kwa sasa, kuna vyuo vikuu viwili kule Pwani ambavyo vinajaribu kutoa mafunzo ya udaktari – Chuo Kikuu cha Pwani kilichoko pale Kilifi na Chuo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}