GET /api/v0.1/hansard/entries/780757/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780757,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780757/?format=api",
    "text_counter": 181,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Baya",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13373,
        "legal_name": "Owen Yaa Baya",
        "slug": "owen-yaa-baya"
    },
    "content": "Kikuu Cha Teknolojia cha Mombasa. Hivyo vyuo vimeshindwa kutoa mafunzo ya matibabu kwa sababu hakuna hospitali ya rufaa na mafunzo. Kama tunataka kuvikuza vyuo hivyo ili viwe taasisi za elimu zinazoheshimika, ni lazima tuhakikishe kwamba mafunzo ya udaktari hayapatikani Nairobi peke yake, bali yanapatikana katika vyuo hivyo pia. Kwa hivyo, tuna wajibu wa kuhakikisha kwa haraka sana kwamba hospitali ya Mombasa imefanywa hospitali ya rufaa na mafunzo kama hospitali za Edoret na Kenyatta. Ni matumaini yangu makubwa kwamba Hoja hii itatiliwa maanani na Serikali. Kabla sijasahau, miongoni mwa maono manne makubwa ambayo Rais Uhuru Kenyatta ametangaza ni matibabu bora kwa kila Mkenya. Ndiyo tuweze kuyafikia malengo hayo, inatubidi sisi Wakenya na Serikali kuhakikisha kwamba hospitali za rufaa pia zimepewa kipaumbele. Rais hawezi kutimiliza ile ndoto ya universal healthcare ambayo iko kwa ile Big Four Agenda yake; hawezi kuafikisha haya maono yake kama ile hopitali ya Mombasa itabakia vile na zile hospitali ndogo ndogo pia zitabakia vile. Ni matumaini yangu hospitali ya Mombasa ikukuzwa kuwa ya rufaa, zile hospitali ndogo ndogo katika Mkoa wa Pwani zitafanya mabadiliko makubwa katika kuhakikisha kwamba watu wa Pwani na Kenya wanapata matibabu yanayofaa ambayo Serikali inatumainia kuyapata."
}