GET /api/v0.1/hansard/entries/780759/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780759,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780759/?format=api",
    "text_counter": 183,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Tuwei",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13436,
        "legal_name": "Vincent Kipkurui Tuwei",
        "slug": "vincent-kipkurui-tuwei"
    },
    "content": "Asante sana Mhe. Spika, kwa lugha ya Kiswahili “Kinara” kwa kunipa nafasi pia, nichangie katika wazo hili ambalo ni la muhimu sana kwa watu wetu na nchi yetu kwa jumla. Hongera mwenzangu, mheshimiwa Jicho Pevu kwa wazo ambalo umelifikiria na kufanya utafiti ambao umeuchukulia kimaanani kwa kutoa maelezo ambayo ni ya kweli. Jambo ambalo ningependa kushukuru ni kwamba tuko na hospitali mbili za rufaa hapa nchini ambazo ni Kenyatta na Eldoret. Lakini, hospitali hizi ziko na shida: wagonjwa ambao wanaletwa pale ni wengi zaidi ya uwezo wa hospitali hizo. Kwa mfano, Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi – Eldoret imekuwa hospital ya pekee; inapokea wagonjwa kutoka sehemu zote, hata kutoka nchi jirani yetu za Uganda, Sudan, Somalia na sehemu zote ambazo zinakaribiana kwa sababu tuko na uwanja wa ndege pale. Jambo ambalo ni nzito ni idadi ya wagonjwa wanaoletwa pale ambao wangepaswa kutibiwa na mahospitali yaliyo karibu. Kwa hivyo, hospitali yenyewe imekosa ule umuhimu wake wa kuwa hospitali ya rufaa. Imekuwa hospitali ya kutibu magonjwa madogo madogo ambayo yangepasa kutibiwa na hospitali zile zingine za kaunti, za Kiwango cha 3 au 2 kule nyuma. Ya pili ni kwamba tuko na tatizo katika jamii kwamba mtu anakuwa mgonjwa zaidi, ikifika kiwango fulani anakimbizwa pale wakati imekuwa kero. Sisi pia kama wananchi tuko na shida. Sisi viongozi ambao tuko hapa tunajua ya kwamba kila wikendi, kila kuchao, sisi ndio tunaitwa kwa michango na matibabu. Nashukuru kwamba afya kwa wote imezingatiwa katika yale mawazo manne ya Rais. Naona itatusaidia zaidi iwapo sisi sote kama vingozi tutaweza kupitisha Mswada na pesa ambazo zitatekeleza wajibu huu wa kupea wananchi wetu afya bora. Cha muhimu ni kwamba ni kweli kwamba tuko na madaktari. Ni kweli kwamba tunaongoza katika eneo hili la Afrika Mashariki kwa upande wa matibabu. Cha muhimu ni kwamba usimamizi wa hospitali zetu na viongozi ambao wameteuliwa kama Mawaziri na makatibu kusimamia kiungo hiki hawajawajibika. Kuna hofu kuhusu dawa ambazo zinaletwa nchini. Madaktari husema kuwa dawa nyingine ambazo zinatumika hazipitii barabara nzuri kwa udhibiti; inachangia wazo la kuongezea magonjwa mengine kama saratani kwa sababu dawa zinaozoingia humu nchini hazipitii utaratibu unaofaa. Inafaa wakati tunaenda kuyapitisha The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}