GET /api/v0.1/hansard/entries/780760/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780760,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780760/?format=api",
    "text_counter": 184,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Tuwei",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13436,
        "legal_name": "Vincent Kipkurui Tuwei",
        "slug": "vincent-kipkurui-tuwei"
    },
    "content": "mambo haya tuyachunguze na kuona ya kwamba kila kitu ambacho tunala kiwe kimepitishwa katika mpangilio ambao utatuepusha na magonjwa. Vile mheshimiwa mwenzangu amesema hapa, maji tunayotumia yana madini ambayo yanasababisha magonjwa mengine. Hili ni jambo ambalo lazima tuliangalie, kama viongozi na nchi. La nne ni kwamba lazima tujiulize tunataka nini kama viongozi. Kila kiongozi anayekuwa Rais angependa kuwacha mambo fulani ambayo atakumbukwa kwayo. Namshukuru mstaafu Rais Moi kwa sababu wazo hili la kuweka Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi mjini Eldoret ni lake wakati wake ule. Tunamshukuru sana. Mungu amusaidie apate ubora wa afya anapozeeka. Hii ni ili sisi sote tujue kwamba ni muhimu tupitishe Hoja hii kwa haraka. Ni jambo ambalo limefanyika jana kwamba hata yeye mwenyewe mstaafu Rais amepelekwa kule atibiwe na hali tuko na uwezo, tumesoma na tuko na rasilimali ambazo tunaweza kutumia kuyakuza mambo haya. Ya mwisho ni kwamba, tulivyo kama nchi, wananchi wakiwa wagonjwa ama wageni wetu wanapozuru nchi, cha muhimu wanachoangalia ni: “Je, nikienda nchi ya Kenya, nipate matatizo ya matibabu, nitapata hospitali ambayo inaweza kunitibu?” Lazima tuwe watu wanapanga mambo yao mbele ili tupate kuimarisha utalii na vile, tupunguze gharama ambazo nchi hii inapitia kwa kuwapeleka wagonjwa wetu nje kwa matibabu. Naunga mkono wazo la kusema kwamba wale wanasimamia hospitali zetu, haswa za saratani, wapeane nafasi kwa nchi nyingine zijenge hospitali hapa; hospitali ambazo zitakuwa nafuu kwetu kwa kutumia teknolojia yao. Nchi ya India iko na matibabu ya gharama ya chini na ya njia bora kuliko nchi zingine ulimwenguni kama Marekani na Ulaya. Nikifunga, hospitlai hizi mbili ambazo tunasema ni za rufaa haziko katika kiwango kimoja. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mishahara ya wafanyakazi wa Kenyatta wa na rufaa ya Eldoret. Daktari wa Kenyatta National Hospital na daktari wa Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi kule Eldoret wana tofauti ya mishahara ya Kshs100,000 na zote ni hospitali za rufaa. Kama hospitali hizi mbili ni za rufaa, lazima mishahara yao isawazishwe kwa sababu inachangia madaktari kutoka kwa hospitali moja kwenda kwa nyingine. Msimamizi wa Kenyatta anashinda msimamizi wa Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi ya Eldoret kwa zaidi ya Kshs200,000 kwa mshahara. Hilo ni jambo la kushangaza sana. Juzi Waziri wa Hazina ya Taifa ambaye anatakiwa kuangalia jambo hili anakalia sana pesa za kupeana huduma za hopitali hizi. Utakuta kwamba hata huduma ya kutolewa kwa hospitali hizi zina shida. Ukiangalia bajeti ya KNH na ya Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi – Eldoret, kuna shida kubwa sana. Ni ombi langu kwa Wizara ya Fedha kuwa pesa za hospitali zitolewe kwa haraka bila kuchelewa ili kupunguza shida ambazo tunapata. Kwa hayo machache, nashukuru."
}