GET /api/v0.1/hansard/entries/780762/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780762,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780762/?format=api",
"text_counter": 186,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanjira",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 769,
"legal_name": "Jane Agnes Wanjira Machira",
"slug": "jane-agnes-wanjira-machira"
},
"content": "Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza Mhe. Mohamed Ali kutoka Eneo Bunge la Nyali kwa kuleta Hoja hii Bungeni. Mengi yamesemwa na sitayarudia, lakini la muhimu sana ni kutimiza Malengo Endelevu ya Maendeleo yanayojulikana sana kama SDGs. Ikiwa hatuwezi kuwapatia wananchi wetu afya njema, basi hatutakuwa tunazingatia malengo hayo. Ukikadiria kuwa watu milioni 44 wanategemea hospitali mbili peke yake za rufaa nchini, utaona kuwa tuna shida. Kwa Mhe. Ali, ningependa kusema, hata ingawa umeileta kama Hoja, usikome hapo kwasababu nilipokuwa Seneti katika Bunge la 11 tulipitisha Hoja nyingi sana na kutekeleza Hoja hizo ambazo si sheria ilikuwa vigumu zaidi. Usikome hapo; leta Mswada tuupitishe katika Bunge hili ili tuwe na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}