GET /api/v0.1/hansard/entries/780763/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780763,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780763/?format=api",
"text_counter": 187,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanjira",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 769,
"legal_name": "Jane Agnes Wanjira Machira",
"slug": "jane-agnes-wanjira-machira"
},
"content": "sheria ambayo itatengewa pesa kwenye Bajeti. Isiwe tu ni kusema na kunena bila kutekeleza. Azimio lilitolewa kule Abuja mwaka wa 2001. Tusiseme tu tuweke viwango fulani vya hospitali ila tuzungumzie uzuri wa hospitali katika kila kiwango. Aidha tuhakikishe pesa zinazowekwa kwenye Bajeti zinalingana na kila kiwango. Nasema hivyo kwa sababu, kwenye Azimio la Abuja, ilisemekana kuwa kiwango cha chini sana cha pesa kiwe ni 15% kwenye Bajeti nzima. Kama nchi bado tuko mbali, lazima tujikakamue kuafikia lengo hilo. Ingawa maeneo mengine ya ugatuzi yamejaribu, hatujafikia kiwango hicho. Hospitali ambazo zimeorodheshwa kama Kiwango 5 ni 12 tu nchini. Ziko Nyeri, Thika, Nakuru, Mombasa, Meru, Kisii na Embu. Walipozigawa, ilikuwa zisambazwe katika maeneo yote nchini. Tusiongeze tu kiwango cha hospitali bila kuongeza madaktari, vifaa vinavyohitajika na pesa kwenye Bajeti. Tunaweza kuanzia mahali ikiwa hizi hospitali 12 tutazifanya kuwa za rufaa. Hospitali ya rufaa lazima iwe hospitali ya rufaa. Hivyo ni kusema yale magonjwa madogo yatibiwe katika zahanati na hospitali za viwango vya kaunti ama kaunti ndogo. Kwa mfano, ile hospitali ya Nakuru PGH ambayo ni kiwango cha tano, iwahudumie watu kutoka maeneo tofauti lakini siyo wagonjwa wa malaria, upangaji wa uzazi, ama homa na mafua. Wagonjwa aina hiyo wapelekwe katika zahanati. Siyo eti ukitaka kupanga uzazi, ama ukitaka dawa za wanaoishi na virusi vya ukimwi unaenda hospitali ya rufaa ya Kenyatta. Dawa hizi zinafaa zipatikane kwenye zahanati. Kwa hivyo, lazima wahudumu wawe waadilifu. Nasema hivi kwa sababu ingawa tunaenda kutimiza hili Lengo Endelevu la Maendeleo la Tatu ama SDG 3 ama ajenda mojawapo ya serikali ya Jubilee, waliopewa kazi kwenye maeneo tofauti nchini⦠Tumeona kwenye magazeti kuwa kuna ufisadi katika utekelezaji wa bima ya NHIF. Kuna shida ya ufisadi wa mamilioni ya pesa. Wakati kuna shida kama hiyo, hatuwezi tukafikia lengo hili. Kuna wakati mtekelezaji mkuu aliachishwa kazi. Madaktari wengi walipopatiwa hiyo kazi walisema hawaitaki kwa sababu inahusishwa na ufisadi kwenye hospitali hiyo. Waliogopa kupakwa tope. Lazima kila mtu akipewa kazi awajibike. Ningependa pia kusema kwamba kama kuna watu ambao wameumia sana kutokana na shida hizi ambazo kila mtu anaongelea ni akina mama na watoto. Ni mwaka wa 2018 na bado tunaongea juu ya vifo vya akina mama zaidi ya elfu kumi ambao hufariki wakati wanajifungua. Ni aibu kubwa kwa taifa. Kama tutaanza na hospitali 12 zilizoko kwenye maeneo tofauti tofauti, tutakuwa tumepiga hatua kubwa. Baadaye, tutaimarisha hospitali kuu katika kila gatuzi nchini. Kwa hayo machache, naunga mkono na kumpongeza tena Mhe. Mohamed Ali kwa Hoja hii."
}