GET /api/v0.1/hansard/entries/780765/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780765,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780765/?format=api",
    "text_counter": 189,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nzengu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13444,
        "legal_name": "Paul Musyimi Nzengu",
        "slug": "paul-musyimi-nzengu-2"
    },
    "content": "Shukrani sana Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia mjadala huu. Kwanza ningependa kumshukuru Mhe. Mohamed Ali kwa kuleta Hoja hii ambayo inamgusa kila mtu. Tukiongea maneno ya siha ama afya, ni jambo linalomlenga kila mwananchi wa Kenya. Sitaki kurudia maneno yaliyosemwa na Wabunge wenzangu, lakini kabla sijachangia sana, ningependa kumkosoa Mhe. King’ara aliyesema Rais Kenyatta ni Rais wa Jubilee. Rais Kenyatta ni Rais wa Kenya na chama cha Jubilee ndicho kilichompeleka mbele akawa Rais. Maneno ya chama sasa yameisha na sisi tuliokua upande huu tumekaribiana sasa. Watu wa Jubilee mjue sasa Rais ni wa Kenya. Nikirudia Hoja iliyoko mbele yetu, ningependa nikubaliane na Mhe. Ali ila nitapendekeza marekebisho machache. Kwa mfano, nitataka arekebishe Hoja kwa kusema, ‘Hospitali ya Mombasa ya Rufaa na Mafunzo’ kwa sababu kuna vyuo vikuu Mombasa ambavyo vinasomesha mafunzo ya afya. Juzi tuliona madaktari wakifanya makosa kwa kumpasua kichwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}