GET /api/v0.1/hansard/entries/780766/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780766,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780766/?format=api",
"text_counter": 190,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nzengu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13444,
"legal_name": "Paul Musyimi Nzengu",
"slug": "paul-musyimi-nzengu-2"
},
"content": "mtu ambaye hakufaa kupasuliwa. Lazima pia tutilie mkazo masomo ya afya. Haiwezekani kuwepo mafunzo ya afya bila kuwepo maabara na hospitali za mafunzo. Nakubaliana na Hoja hii kwa sababu gharama ya kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi kama vile India, Tel Aviv… Tunayo habari kwamba aliyekuwa Rais wetu yuko Tel Aviv. Hivi juzi kiongozi wa chama chetu cha Wiper alikuwa ujerumani akakaa kule kwa miezi kadhaa. Tunajua kwamba ni wengi wetu ambao wamekuwa wakienda nchi za nje kutafuta matibabu. Naomba tutengeneze hospitali zetu za rufaa hata kama watalaamu hatuna wengi, tuwalete kutoka nchi za nje, tuwakodeshe kwa miezi au miaka kama tulivyokodesha vifaa vya kutibia ugonjwa wa saratani. Labda ule muda uliyopeanwa wa kukodi vifaa vile ufupishwe na ukiisha tuangalie namna ya kununua vifaa vyetu. Hii ni kwa sababu nimeelezwa kwamba hata vifaa vidogo vidogo kama makasi sharti tuvinunue sasa. Kwa hivyo, ningeomba turekebishe namna ya kukodesha vifaa vya kutibu saratani. La mwisho, nimeiskia kutoka kwa wale Wabunge waliokuwa Bunge la 11 kuwa kuna Hoja na sheria nyingi zilipitishwa kama vile Mhe. Mwadime na Mbunge wa Meru walivyosema. Naibu Spika wa Muda, ningeomba kama inawezekana uitishe hiyo Miswada ama Hoja ili tuchukue likizo ama nafasi tuzizungumzie na tuipe ile kamati tekelezi jukumu hilo. Mwisho kabisa, ningependa kuwashukuru wanafunzi wa Shule ya Upili ya Kamuwongo ambao wametembelea Bunge hili leo. Ni shule katika eneo langu la Bunge. Hao ni viongozi wa kesho watakaokuwa Wabunge kama mimi. Asante sana, Naibu Spika wa Muda."
}