GET /api/v0.1/hansard/entries/780770/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780770,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780770/?format=api",
"text_counter": 194,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ali Sharif",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Naibu Spika wa Muda, kabla ya kuendelea, nilikuwa nimeomba hoja ya nidhamu kuhusiana na suala hili nzima. Hoja hii inaonekana imetia hamasa wengi na wangependa kuchangia lakini naona muda haupo nasi maana umetupa kisogo. Pengine kupitia utaratabu wa Bunge hili, Sheria za Bunge, Kifungu Nambari 97(4), ningeomba muda wa kuongea pengine upunguzwe kutoka dakika kumi hadi tano ili wenzetu wengine nao waweze kupata fursa ya kuchangia ikiwa itawezekana. Naibu Spika wa Muda, ningependa kumpongeza Mhe. Ali kwa fikira ya kuleta Hoja hii hapa.Vile vile, ningependa kumpongeza kwa ule utafiti ameweza kufanya kikamilifu kuhusiana na suala nzima la afya katika nchi yetu ya Kenya. Pengine kadri tunavyoendelea kujadili suala hili ndivyo tutakapoweza kuuliza tatizo liko wapi na limesababishwa na nini. Hii ni kwa sababu, linaonekana kama kwamba katika karne hii ambayo tuko, wengi wanaochangia swala hili hawajaridhishwa na huduma ya afya nchini Kenya. Vile vile, tunajua kuwa ni pesa nyingi ambazo zinatumika katika nyanja hii ya afya hususan baada ya Wakenya kusema kuwa huduma hizi zipelekwe mashinani na zigatuliwe. Ningependa kushukuru wale wahusika mashinani ambao wameweza kushughulikia suala hili kwa namna ambavyo wameweza kufanya. Lakini, tatizo hili bado lipo na wakenya wengi wanateseka. Sio kwamba pengine nitazungumzia eneo Bunge langu la mashinani bali hata Nairobi kuna watu wanaoishi humu lakini wakishikwa na homa hawajui waende wapi ama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}