GET /api/v0.1/hansard/entries/780771/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780771,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780771/?format=api",
"text_counter": 195,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ali Sharif",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "watasaidika namna gani. Kama nilivyosema, kuna umuhimu wa kuangalia suala hili na kuliangazia kwa undani kabisa. Tatizo ni nini na limesababishwa na nini? Naibu Spika wa Muda, Hospitali ya Mombasa kwa hivi sasa hakuna asiyejua kwamba inapokea wageni kupitia kila sehemu katika masuala ya matibabu. Iwe ni wageni kutoka Lamu, Kilifi ama sehemu tofauti, wote huenda Hospitali ya Mombasa. La kusikitisha ni kuwa Bunge hili likikaa kugawanya pesa za mashinani ama za kaunti ama kugawanya pesa katika Bajeti yake kila mwaka, sijaona mambo haya yakifikiriwa. Jambo ambalo ningependekeza tunaposubiri ujenzi ambao umependekezwa wa hospitali nyingine kule Mombasa, tayari hospitali hii inahudumia na kupeana huduma ambayo tuko nayo. Tatizo tu ni kwamba huduma hizi haziwezionekana kukamilika ikiwa Bajeti ya nchi hii haiweki kisawasawa na kusema kwamba kwa sababu fulani tumepea hospitali ya Mombasa bajeti ya ziada ili iweze kujimudu na mambo kama haya huku tukipanga namna jinsi tutakavyojenga hospitali nyingine ya Level 6. Kadri tunavyoendelea kuishi katika nchi hii, tukumbuke pia kwamba idadi ya watu inaongezeka. Idadi ya watu ikiongezeka kuna dharura ya mambo yanayoweza kupanuliwa ili yaongezeke. Naibu Spika wa Muda, suala lingine lililojadiliwa ni suala la madaktari. Mhe. Ali amepeana idadi ya madaktari walioko Kenya. Pengine, tujiulize ni kwa nini madaktari ni wachache hivyo. Pia, ni kwa nini hao madaktari hawana imani ya kufanya kazi Kenya hii. Hayo ndiyo mambo tunayotaka kuyajua ili tuyatafutie suluhisho. Madaktari wengi wanaosomea taaluma hii huenda kufanya kazi nchi za nje kwa sababu malipo huku ni duni. Kwa hivyo, suala la malipo kwa madaktari ni kitu muhimu sana kitakachofanya madaktari wawe na imani na utulivu wa kufanya kazi hapa Kenya. Vile vile, inawagharimu pesa nyingi sana wale wanaosomea udaktari. Hivyo basi, ningeomba Serikali iwe na mipangilio maalum ya kuwasomesha takriban vijana 500 wanaotaka kusomea taaluma hii ili idadi ya madaktari iongezeke kadri idadi ya watu inavyoongezeka. Naibu Spika wa Muda, matatizo ni mengi. Kuna haja ya kuhakikisha mwananchi wa kawaida amepata huduma hizi. Ingawaje Serikali bado inajitahidi, bado kuna tatizo. Tatizo kubwa lipo katika wahusika wakuu ambao wanaendeleza mambo haya. Kama viongozi, tunafaa kusimama kidete na kuyaweka mambo kama haya sawasawa. Mambo mengi huzungumzwa hapa lakini ukienda mashinani hakuna hata moja limeweza kufanyika. Kuna dharura ya Wakenya kusaidika kiafya kwa sababu rasilimali ya kiumbe chochote ni afya. Sisi kama binadamu tunafikiria pengine rasilimali zetu kubwa ni masuala ya pesa lakini jambo muhimu sana ni afya ya binadamu. Tunahitaji kuizingatia pakubwa na kuhakikisha tumefuatilia haya na yamekuwa sawa kwa wale wenzetu wanyonge, vile ilivyozungumzwa kuhusu wale hawawezi kujimudu kupata matibabu ya gharama za juu. Naibu Spika wa Muda, kuna watu ambao hawajielewi katika nchi hii. Mtu anaamka asubui na hajui atajisaidia namna gani na familia yake huku tayari kuna uzito wa magonjwa na kadhalika. Kwa hivyo, kama nchi pia tujaribu kuangalia uchumi wa watu wetu ili kuwasaidia kupambana na mambo kama hayo ya magonjwa yanapofika. Ningependa kuunga mkono na ningependa Bunge hili liwe pamoja ili kupitisha Hoja hii. Tuweze kufuatilia jambo hili na kuhakikisha kwamba Mkenya wa kawaida anasaidika na haya tunayozungumzia hapa. Asante."
}