GET /api/v0.1/hansard/entries/780780/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780780,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780780/?format=api",
"text_counter": 204,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Asha Mohamed",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13262,
"legal_name": "Asha Hussein Mohamed",
"slug": "asha-hussein-mohamed"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja ya kiongozi mwenzangu, Mbunge wa Nyali, Mohamed Ali, kama mama kiongozi wa Mombasa Kaunti. Hospitali kuu ya Pwani ambayo iko Mombasa Kaunti inahudumia mkoa wa Pwani na kutoa huduma ya afya. Kwa hivyo, Hoja hii ya ndugu yangu Mohamed in muhimu ili tuweze kujenga hospitali ya rufaa na kuhakisha kwamba itapatiwa kipaumbele ili pia iwe na chuo kikuu. Hivi juzi nimerudi kutoka Ujerumani ambako nilipata matibabu mazuri sana katika Chuo Kikuu cha Ujerumani. Kwa hivyo, tukiweza kupatia hospitali zetu fedha na kuziinua katika kiwango kinachofaa ili wananchi wapate huduma, itakuwa vizuri. Zaidi, huko Hospitali kuu ya Pwani na pia zahanati zingine kuna shida kubwa ya linda mama. Ningependa tuhakikishe kwamba linda mama inafwatiliwa haraka ili akina mama waweze kupata huduma zaidi katika zahanati zote huko Mombasa na Kenya kwa jumla. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}