GET /api/v0.1/hansard/entries/780795/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780795,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780795/?format=api",
"text_counter": 219,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nassir",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ahsante ndugu yangu, Mhe. Mohamed Ali. Nataka kulikumbusha Bunge hili kuwa katika Bunge lililopita kuna Mswada nilioleta kubadilisha sheria na kuifanya Coast General Hospital ijulikane kama Pwani Referral Hospital. Nataka kutoa sababu. Wengi wametaja kuwa hospitali kuu zenye kusimamiwa na serikali ni mbili. La, si mbili. Ni nne. Ya kwanza ni Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta yenye wafanyakazi 6,000 na vitanda 800 lakini mpaka watu 3,000 wanaweza kulala katika hospitali hiyo. Ya pili ni Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi ambayo ilipandishwa ngazi mwaka 2010. Wakati inafanyiwa census, wafanyakazi wake walikuwa 3,066. Nataka kutoa hesabu. Katika hesabu ya fedha ya Bajeti ya mwaka 2014/2015, Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta ilipewa Ksh6.5 bilioni. Mwaka wa 2015/2016 ilipatiwa Ksh6.6 bilioni. Katika mwaka wa 2014/2015, Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi ilipewa Ksh4.3 bilioni na mwaka wa 2016/2017 ikapewa Ksh 4.7 bilioni. Mathare Hospitali ni hospitali ya watu wenye akili punguani. Hospitali ya mwisho ilijengwa wakati wa ukoloni mwaka wa 1945. National Spinal Injury Hospital ina vitanda 25 pekee. Kwa hivyo, sio hospitali mbili mbali ni nne ambazo Serikali kuu inaweza kuangalia."
}