GET /api/v0.1/hansard/entries/780798/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780798,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780798/?format=api",
    "text_counter": 222,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13398,
        "legal_name": "Amin Deddy Mohamed Ali",
        "slug": "amin-deddy-mohamed-ali"
    },
    "content": "Shukrani sana, Mhe. Spika wa Muda. Labda kwa kuhitimisha katika Hoja hii ya siku ya leo ambayo imechangiwa vilivyo, kwanza kabisa nawashukuru Wabunge wenzangu walioweza kuchangia na wale wote ambao walikuwa wanataka kuchangia lakini muda haukuwaruhusu. Ningependa pia kuwaambia kuwa Hoja hii ni ya taifa. Asilimia 80 ya Wakenya wana matatizo ya afya. Hoja hii bila shaka itakapofaulu na kufanywa sheria, itaweza kuhakikisha ya kwamba kila kaunti nchini Kenya imepata hospitali ya Level 6 ama hospitali ya rufaa."
}