GET /api/v0.1/hansard/entries/780799/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780799,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780799/?format=api",
"text_counter": 223,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13398,
"legal_name": "Amin Deddy Mohamed Ali",
"slug": "amin-deddy-mohamed-ali"
},
"content": "Tumeweza kutoa takwimu mbalimbali na kuonyesha ni kwa nini tunahitaji hospitali hizi. Rais Uhuru Kenyatta mapema mwaka jana alisema ya kwamba anatoa pendekezo la kujengwa kwa hospitali katika kila kaunti. Kwa wale ambao waliingia wakati ambapo nilikuwa nikiendelea ama walichelewa kuingia, niliwapatia mifano mbalimbali na kuwaambia ya kwamba sisi tunaenda kinyume na Shirika la Afya Duniani (WHO). Shirika hilo linasema kuwa daktari mmoja anapaswa kuwashughulikia wagonjwa 1000. Hapa Kenya daktari mmoja anawashughulikia wagonjwa 10,000. Watu wanaumia sana. Tunazidi kumaliza kizazi. Tunazidi kuhakikisha ya kwamba watu wetu wanazidi kuumia badala ya kuwawakilisha katika Bunge. Tunawawakilisha katika mambo mengine yasiyo na maana. Naomba Bunge hili liweze kupitisha Hoja hii na kujua ya kwamba tuko tayari kukataa kuongeza majeneza Kenya ili tupunguze mzigo huu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}