GET /api/v0.1/hansard/entries/780800/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780800,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780800/?format=api",
"text_counter": 224,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13398,
"legal_name": "Amin Deddy Mohamed Ali",
"slug": "amin-deddy-mohamed-ali"
},
"content": "Ningependa kuwapongeza akina mama Wabunge wenzangu ambao mara kwa mara nawaona kwenye runinga wakati ambapo mama amepigwa katika visa vya nyumbani ama amebakwa, wanakimbia katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta kusimama naye. Leo nawataka msisimame nyuma ya mama huyo lakini msimame nyuma ya hospitali ili huyo mama asipate shida kutolewa Wajir mpaka Nairobi mbali apate huduma hizo hapo. Kwa hivyo, naona muda ndio huo umefikia kikomo. Langu nikusema tu asanteni sana na natumai idadi ya madaktari itaongezeka na hospitali zitajengwa. Kwa Wabunge wote, nasema asanteni sana na Mungu awabariki."
}