GET /api/v0.1/hansard/entries/780834/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780834,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780834/?format=api",
"text_counter": 27,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "KWAMBA, tukifahamu Kifungu cha 43 cha Katiba ya Kenya kimeweka wazi kwamba kila Mkenya ana haki ya kuwa na kiwango bora cha afya kinachojumuisha afya bora ya uzazi; aidha, katika utaratibu wa ajenda ya maendeleo ya baada ya Mwaka wa 2015, dunia imewajibikia afya kwa wote na kutimiza Lengo Endelevu la Maendeleo la tatu (SDG-3) kuhakikisha na kuendeleza maisha na afya bora kwa wote; tukiafiki, uwekezaji katika sekta bora ya afya ni muhimu kuhakikisha kila mtu anapata huduma za kimsingi za afya bila kuzingatia eneo analotoka au hali yake ya kiuchumi; tukitambua, asilimia 80 hutegemea huduma ya afya ya umma ilihali kuna hospitali mbili pekee za rufaa nchini ambazo ni Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta - Nairobi na Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi - Eldoret; tukizingatia, Kifungu cha ishirini na tano (25) kikiambatanishwa na Mpangilio wa Kwanza wa Sheria ya Afya, 2017, kinasema kutakuwa na hospitali ya kitaifa ya rufaa katika kila gatuzi (Level 6); Bunge hili linahimiza Serikali kuharakisha kuwepo Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa katika Kaunti ya Mombasa ili kufanikisha huduma zote za afya zinazohitajika eneo hilo zitumiazo teknolojia pevu na wataalamu wa hali ya juu pamoja na kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya kabla na baada ya kuhitimu."
}