GET /api/v0.1/hansard/entries/781107/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 781107,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/781107/?format=api",
    "text_counter": 300,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Ni mimi ambaye alizindua ndoto hii ambayo imetimia. Punde tu baada ya uchaguzi, nilisema hadharani kwamba itakuwa muhimu Rais Uhuru Kenyatta, ambaye alikuwa ameshinda uchaguzi, na Mhe. Raila Odinga, ambaye alikuwa hakupoteza bali mambo yalikuwa yamemwendea mrama, kushirikiana. Nilisema kitumbua cha Mhe. Raila kilikua kimeingia mchanga kidogo, na hivyo basi akae na Rais Uhuru Kenyatta wawaunganishe Wakenya. Mhe. Raila ana sifa zake. Ni lazima tumheshimu. Ni kigogo na uti wa mgongo wa siasa za taifa la Kenya. Hakuna jinsi Rais Uhuru angefanya kazi bila kuungana na Mhe. Raila. Hii inatufunza nini? Inatufunza kwamba ukipenda, usipende sana, na ukichukia, usichukie sana. Usitusi wakunga kama uzazi ungalipo."
}