GET /api/v0.1/hansard/entries/781239/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 781239,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/781239/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante sana, Bwana Spika. Swala la SGR ni nyeti sana kwa sababu linaathiri watu kutoka Mombasa mpaka labda Naivasha wakati itakamilika. Ijapokuwa SGR kwa sasa inafanya kazi, kuna baadhi ya watu ambao wameathirika kutoka sehemu ya Mombasa 001 mpaka 020 ambao hawajalipwa ridhaa kwa ardhi zao zilizochukuliwa kwa maswala ya SGR. Vile vile, kuna sehemu ya baharini kule Eneo Bunge la Changamwe ambapo mikoko na miti mingine ya thamani imeharibiwa na mpaka sasa, hakujakuwa na njia yoyote ya kurekebisha madhara kama yale ambayo yametokea kwa mazingira. Kwa hivyo, ninaunga mkono Petition ya watu wa Kajiado. Imekuja kwa wakati mwafaka kwa sababu kuna sehemu zingine ambazo hazijaathirika na mradi huu wa SGR ambazo zitakuwa muhimu kwa watu kuzichunguza kwa makini. Pia, wanafaa kuona kwamba yale madhara yanayosababishwa na mradi huu yanaweza kupunguzwa na wananchi wapate mradi bila kupata madhara ya mazingira. Asante sana, Bwana Spika."
}